SiasaAsia
Shambulio la bomu laua watu 34 Pakistan
5 Machi 2025Matangazo
Awali magaidi walivamia kambi ya kijeshi iliyoko Bannu katika wilaya ya mkoa wa kaskazini-magharibi wa Khyber Pakhtunkhwa, shambulio lililofanyika jioni wakati watu walipokuwa wakifuturu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Wanajeshi 18 wameuwawa katika mapambano na wanamgambo nchini Pakistan
Kitengo cha habari cha jeshi la Pakistan ISPR kimeeleza kuwa magaidi wote 16, wakiwemo washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga wameuawa, na kuongeza kuwa shambulio hilo lilizimwa kutokana na ufanisi wa majibu ya vikosi vya usalama.
Katika miezi ya hivi karibuni, ghasia zimeongezeka huko Pakistan wakati vikosi vya nchi hiyo vikizidisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Taliban.