Shaka shaka kuhusu kuhalalika uchaguzi wa Iran:
1 Februari 2004Matangazo
TEHERAN: Baada ya Baraza la Ukaguzi wa Maslahi ya Dola kuamua kuruhusu kiwango fulani tu cha wanasiasa wa kimageuzi kugombea katika uchaguzi mkuu ujao, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema anatiia shaka ikiwa unahalalika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Februari. Kwa mara nyingine alitoa mwito wa kuakhirishwa uchaguzi huo. Kufuatana na hali ya sasa haiwezekani kufanya uchaguzi huru alisisitiza Waziri huyo wa Mambo ya Ndani Abdolwahed Mussawi-Lari. Japokuwa Baraza hilo la Ukaguzi hapo jana lilibatilisha sehemu ya uamuzi wake wa kuwazuiya wagombea wanaounga mkono mageuzi kushiriki katika uchaguzi mkuu, lakini lilikataa kukubalia mwito wa kuakhirishwa uchaguzi. Wabunge kadha wa kimageuzi wanadhamiria kujiuzulu na kuugomea uchaguzi.