Serikali ya Ujerumani inavyoundwa na kansela
17 Septemba 2009Kansela pamoja na baraza lake la mawaziri kwa pamoja wanaunda serikali ya Ujerumani, ikiwa ni uongozi wa kisiasa wa nchi. Kazi yao ni kutekeleza sheria zilizopitishwa na bunge pamoja na kuiwakilisha nchi nchi za nje.Bunge linakazi ya kushauri na kuamua kuhusu sheria za nchi. Kwa mujibu wa katiba ya Ujerumani , kansela anawajibu kwa upande mmoja kueielekeza nchi katika njia sahihi ya kisiasa.Kwa upande mwingine baraza la mawaziri linaamua masuala mbali mbali kwa kupiga kura. Madaraka ya kansela yanategemea wingi serikalini na makundi ya upinzani katika bunge.
Ni katika wakati wa kujihami ndipo kansela anaweza pia maelekezo na amri ya kuingia vitani kwa jeshi la Ujerumani. Katika wakati wa amani waziri wa ulinzi ndio mwenye madaraka kwa jeshi la Ujerumani. Wananchi wa Ujerumani hawawezi kumchagua kansela moja kwa moja, lakini wanauwezo wa kuamua kila baada ya miaka minne kuhusu nani anafaa kuwa kansela katika uchaguzi mkuu wa Ujerumani. Ili kuwa kansela, ni lazima anayetaka kuchaguliwa kuwa kansela apate wingi wa wabunge wa kuchaguliwa katika bunge, hii ni kile kinachoitwa, wingi wa kansela. Kwa hiyo ni lazima chama cha mtu anayetaka kuwa kansela , kisheria atafute mshirika wa kuunda nae serikali. Kimsingi serikali ya mseto nchini Ujerumani huundwa na vyama viwili tofauti.
Wakati kansela akifanikiwa kupata mshirika wa kuunda serikali, anaingia katika kazi ya kupanga baraza lake la mawaziri. Anaamua ni maeneo gani ya kisiasa ni muhimu na mawaziri gani anataka kuwa nao katika serikali yake. Nyadhifa muhimu ni pamoja na uchumi, mazingira, mambo ya ndani, mambo ya kigeni, fedha na ulinzi, lakini hata pia familia, sheria, usafirishaji na afya. Mawaziri wanaongoza wizara kwa kuwajibika binafsi, kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa.
Kansela anawataja mawaziri, aliowateua, ambapo katika utaratibu vyama ndio vimeamua kuhusu wizara watakazotumikia. Baada ya hapo ni kazi ya rais wa shirikisho kuweza kumthibitisha kansela mtarajiwa kuwa kansela kamili. Kansela huchaguliwa na wabunge wa bunge la Ujerumani. Hi lakini ni baada ya matayarisho ya kuunda serikali kukamilika, wizara kutayarishwa na mawaziri kupangwa.
Kansela anaweza kuondolewa madaraka kwa kupitia kura ya kutokuwa na imani nae, pale tu bunge kwa wingi mkubwa kumchagua mtu mwingine kuwa kansela, ama kutokana na kushindwa kwa kura ya kutokuwa na imani na rais wa shirikisho kulifuta bunge.
Chama kimoja huunda kundi la upinzani bungeni. Kutokana na nguvu yake hupata nafasi ya kuwa kiongozi wa tume za kudumu na za muda za bunge. Hapa kazi za bunge zinakuwa zimetekelezwa, hususan ushauri kuhusu miswada ya sheria, hoja na maulizo.
Bunge pia linamchagua rais wa shirikisho. Ni wadhifa wa pili katika utawala wa nchi, na pia baada ya kansela rais ndio kiongozi wa nchi. Spika wa bunge kwa kawaida anachaguliwa kutokana na chama chenye wingi mkubwa bungeni, anawakilisha bunge, anaongoza vikao na kuangalia kuwa haki za wawakilishi zinalindwa.
Katika bunge la majimbo Bundesrat , wawakilishi wa majimbo wanaunda baraza la wawakilishi wa majimbo. Katika baraza hilo kunaingia viongozi 16 wa serikali za majimbo pamoja na mawaziri wa majimbo. Kila jimbo lenye wakaazi wengi linakuwa na kura nyingi katika bunge hili la majimbo Bundesrat.Majimbo madogo kama Bremen kwa mfano wanakura tatu, na majimbo makubwa kama Bayern yanakura sita.
Mwandishi Hanno Schiffer / ZR/ Kitojo Sekione
Mhariri Mohammed Abdul-Rahman