Uhamiaji waisambaratisha serikali ya Uholanzi
3 Juni 2025Wilders alitishia kukiondoa chama chake cha PVV siku ya Jumapili hadi pale muungano huo wa vyama vinne utakapokubaliana na mahitaji yake ya kuwekwa kanuni kali dhidi ya waomba hifadhi.
"Kama mnavyojua, PVV iliwaahidi wapiga kura sera kali zaidi ya hifadhi na kuwa miongoni mwa nchi zenye sheria kali zaidi barani Ulaya. Tulipendekeza katika mpango wa kufunga mipaka, kuwazuia, kuwafukuza na kutojenga vituo vingine vya waomba hifadhi. Tuliuwasilisha huo mpango na tuliwaomba washirika wetu watuunge mkono. Hawakufanya hivyo. Kwa hiyo sitaweza kufanya chochote kwa sasa zaidi ya kusema kwamba tumejiondoa kwenye baraza hili."
Mpango wa chama chake wenye vipengele 10 ulijumuisha hatua kama vile kufungwa kwa mipaka na vituo vya kuwapokea waomba hifadhi, kuhitimisha mpango wa kuziunganisha familia za wakimbizi waliotambuliwa.