Serikali ya Ufaransa hatarini kuanguka katika kura ya imani
8 Septemba 2025Matangazo
Waziri Mkuu wa nne wa Ufaransa katika kipindi cha miaka mitatu François Bayrou, anakabiliwa na hali ya kukaribia kushindwa kwa hakika katika kura ya imani hivi leo.
Viongozi wa upinzani katika nyanja ya kisiasa kote Ufaransa wameweka wazi kwamba watapiga kura kumuondoa waziri mkuu huyo.
Matokeo ya kura hiyo iliyopangwa kufanyika mchana yanatarajiwa kuitumbukiza Ufaransa, nchi ya pili kwa ukubwa kiuchumi barani Ulaya katika sintofahamu ya kisiasa na kuzidisha mkwamo katika wakati mgumu kwa bara la Ulaya ambalo linatafuta umoja katika kukabiliana na vita vya Urusi nchini Ukraine, misuaguano ya kibiashara na Marekani na China inayoendelea kujiimarisha.