Marekani yakosoa AfD kuorodheshwa taasisi ya itikadi kali
3 Mei 2025Matangazo
Chama hicho kinajiita chama mbadala kwa Ujerumani. Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance ameituhumu Ujerumani kwa hatua hiyo amesema inaujenga upya ukuta wa Berlin.
Soma zaidi: AfD yaorodheshwa kuwa taasisi inayofuata itikadi kali
Naye Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Marco Rubio amesema si demokrasia kwa shirika la ndani la ujasusi la Ujerumani kupewa nguvu ya kukifuatilia kwa karibu chama hicho cha upinzani.
Kitendo cha AfD kuwekwa kwenye orodha ya taasisi zenye itikadi kali kama ilivyotangazwa Ijumaa, kitazirahishia zaidi mamlaka za Ujerumani kutumia njia za siri kama vile kuwapenyeza watu wake katika kukichunguza na kufuatilia mawasiliano yake.