Serikali ya Trump yaanza kutekeleza ushuru mpya
7 Agosti 2025Serikali ya Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump imeanza kutekeleza mpango wake wa kutoza ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka nchi mbalimbali baada ya miezi kadhaa ya vitisho.
Ushuru wa uagizaji wa bidhaa wa kuanzia asilimia 10 hadi 50 sasa utatumika kwa bidhaa zinazosafirishwa hadi Marekani. Washirika wakuu wa kibiashara wa Marekani na wanakabiliwa pia na viwango vya juu vya ushuru ikiwemo Umoja wa Ulaya utakaolipa asilimia 10 au zaidi na asilimia 15 itakayotozwa kwa bidhaa za Japan.
Akiutumia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump amepongeza kuanza kutekelezwa kwa hatua hiyo akisema Marekani sasa itanufaika kwa kupata mabilioni ya dola. Kiongozi huyo mara zote amekuwa akiamini kwamba Marekani imekuwa haitendewi haki katika ulingo wa biashara ya kimataifa.
Hata hivyo, hatua hiyo inatajwa kuwa inafungua uwanja mpya wa vita vya kibiashara.