Serikali ya Syria yaanza kuhamisha familia za Bedui
21 Julai 2025Mabasi yaliyojaa familia za jamii ya Bedui yaliandamana na magari ya Shirika la Hilali nyekundi la Syria pamoja na magari ya kubeba wagonjwa. Baadhi ya familia ziliondoka kwa malori zikiwa zimebeba mali zao.
Zaidi ya watu 1500 wa jamii ya Bedui wamehamishwa Sweida
Waziri wa mambo ya ndani wa Syria Ahmad al-Dalati ameliambia shirika la habari SANA kwamba mpango huo pia utawezesha watu waliopoteza makazi kutoka Sweidakurejea, kwasababu mapigano hayo yamesitishwa kwa kiasi kikubwa na juhudi za kusitisha mapigano kabisa zinaendelea.
Hali mjini Sweida inaripotiwa kuwa tulivu baada ya kushuhudiwa mapigano makali ya kidini
al- Dalati ameongeza kusema kuwa wameweka vizuizi vya usalama katika eneo la Sweida ili kuweka ulinzi na kusimamisha mapigano katika eneo hilo. Usitishaji mapigano ulitangazwa Jumamosi katika mkoa huo wa Sweidana kumaliza machafuko ya kimadhehebu yaliyosababisha mauaji ya zaidi ya watu 1,100 katika kipindi cha wiki moja.