Serikali ya Myanmar yatangaza wiki ya maombolezo
31 Machi 2025Katika taarifa, mamlaka ya kijeshi nchini humo, imesema bendera za kitaifa zitapeperushwa nusu mlingoti hadi Aprili 6 kuwaomboleza watu waliopoteza maisha pamoja na uharibifu uliotokana na tetemeko hilo la ardhi .
Idadi ya walioangamia kufuatia tetemeko la ardhi Myanmar inazidi kupanda
Tangazo hilo limetolewa katika wakati ambapo kasi na udharura wa juhudi za uokoaji zinaendelea kufifia huko Mandalay, mojawapo ya miji iliyoathiriwa zaidi na wa pili kwa ukubwa nchini humo, wenye zaidi ya wakazi milioni 1.7.
Hali ni mbaya mjini Mandalay
Msimamizi mkuu wa msikiti wa Sajja kaskazini mwa Mandalay Aung Myint Hussein, amesema hali ni mbaya sana na kwamba ni vigumu kueleza kinachoendelea.
Tetemeko jengine laupiga mji wa Mandalay, Myanmar
Watu walipiga kambi usiku kucha katika barabara kote mjini humo, ama kwa kushindwa kurejea makwao au kwa kuwa na wasiwasi wa kutokea tena kwa mitetemeko iliyolikumba jiji hilo mwishoni mwa wiki iliyopita.