Kongo na M23 kushiriki mazungumzo ya amani nchini Angola
17 Machi 2025Msemaji wa rais wa Felix Tshisekedi wa Kongo Tina Salama na msemaji wa kundi la M23 Laurence Kanyuka wamesema wajumbe wa pande hizo mbili wametumwa mjini Luanda tayari kushiriki mazungumzo hayo ya moja kwa moja.
Wakati huohuo, Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean Noel Barrot ametoa wito wa usitishwaji mapigano huko Kongo.
" Kwa sasa, ni lazima usitishaji mapigano uanzishwe mara moja ili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, makundi ya waasi na Rwanda wafanye mazungumzo kuelekea amani ya haki na ya kudumu katika ukanda huo."
Soma pia:Bunge la Kongo lajadili mzozo wa mashariki mwa nchi
Mazungumzo ya amani kati ya Kongo na Rwanda yalivunjika bila kutarajiwa mwezi Desemba mwaka jana, baada ya Rwanda kuweka sharti la kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kongo na waasi hao wa M23 ambao inadaiwa wanaungwa mkono na Rwanda, jambo ambalo lilitupiliwa mbali na serikali ya Kongo.