Utawala nchini Mali wasitisha shughuli za vyama vya kisiasa
14 Mei 2025Waziri anayehusika na mageuzi ya serikali, Mamani Nassire, ametangaza uamuzi huo kupitia taarifa iliyotolewa kwenye televisheni ya taifa.
Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwepo na jaribio la mara kwa mara la kupinga kusitishwa kwa shughuli za vyama vya kisiasa nchini humo.
Soma pia: Wataalamu wa UN wahimiza uchunguzi wa mauaji ya halaiki Mali
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeukosoa uamuzi huo, likisema ni pigo jingine kwa demokrasia nchini Mali.
Mnamo mwezi Aprili, mawaziri walipendekeza muda wa kiongozi wa kijeshi Assimi Goita uongezwe hadi mwaka 2030.
Goita ambaye aliingia madarakani kupitia mapinduzi mawili ya kijeshi mwaka 2020 na 2021, ameahidi kuandaa uchaguzi japo mipango hiyo imeahirishwa kwa "sababu za kiufundi" bila ya kutolewa muda maalum wa kufanyika kwa uchaguzi huo.