Serikali ya Iraq yaendeleza mazungumzo kuhusu katiba:
29 Februari 2004Matangazo
BAGHDAD: Nchini Iraq serikali ya mpito iliyowekwa na Marekani imeendeleza mazungumzo yake kuhusu katiba mpya ya mpito iliyokuwa ikabidhiwe hapo Jumamosi ya jana. Msemaji wa utawala wa Kimarekani alisema haitazamiwi kuwa katiba hiyo mpya ya mpito itaweza kuwafikiwa kabla ya Jumatano. Serikali ya mpito inataka kungojea mpaka imalizike sherehe ya ASHURA ya Washiya, alisema msemaji huyo. Serikali hiyo ya mpito ya wajumbe 25 inashauriana tangu Ijumaa juu ya mfumo wa katiba mpya ya mpito iliyokusudiwa kutumika mpaka itakapochaguliwa serikali rasmi. Inatazamiwa kuwa katiba hiyo itatuwama juu ya misingi ya mfumo wa kidemokrasi. Mojawapo ya vituo vya ubishi vinahusiana na tasfiri ya sheria ya Kiislamu katika katiba mpya. Nchini Iraq leo aliuawa mwanajeshi mwengine wa vikosi vya mwungano.