Bangladesh yasema haina nia ya kukifuta chama cha Hasina
21 Machi 2025Uamuzi huo unaiweka serikali hiyo kwenye msuguano na wanafunzi waliopambana kuuangusha utawala wa Hasina mwaka uliopita.
Chama cha Hasina cha Awami League kinashutumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu wakati wa utawala wa miaka 15 wa kiongozi huyo, ikiwemo matumizi ya nguvu wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwaka jana.
Soma pia:Je, India itamrudisha Sheikh Hasina Bangladesh?
Viongozi wa wanafunzi ambao bado wanaomboleza vifo vya wenzao miongoni mwa zaidi ya watu 800 waliopoteza maisha kwenye maandamano hayo, wanashinikiza chama hicho kipigwe marufuku.
Hata hivyo kiongozi wa serikali ya mpito nchini huko Muhammad Yunus amekataa shinikizo hilo lakini ameahidi viongozi wa chama hicho wanaotuhumiwa kutenga uhalifu ikiwemo mauaji watafikinywe mbele ya vyombo vya sheria.