Serikali Ujerumani yaunga mkono kushushwa bei ya umeme
3 Septemba 2025Matangazo
Waziri wa Uchumi Katherina Reiche amesema uamuzi huo wa baraza la mawaziri - ambao bado unahitaji idhini ya bunge - ni habari njema kwa watumiaji umeme Ujerumani.
"Tunaurahisisha mzigo wa watumiaji, tunaurahisisha mzigo kwa makampuni," alisema Reiche.
Ujerumani imepitia kipindi kigumu cha bei ghali za umeme tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Na sasa mpango huo unaweza kuikoa familia ya wastani hadi yuro 100 za malipo ya umeme kwa mwaka, kulingana na hesabu za serikali.