Serikali ya DRC na waasi wa M23 warudi Doha
26 Agosti 2025Matangazo
Wajumbe wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa kundi la M23 wamerejea tena kwenye meza ya mazungumzo mjini Doha.
Hayo yameelezwa na wajumbe hivi leo kufuatia ripoti za kuzuka machafuko katika eneo la mzozo la mashariki mwa Kongo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Qatar, Majed al Ansari, amewaambia waandishi habari mjini Doha, kwamba wajumbe wa pande hizo mbili waliofika Qatar, watajadili kuhusu utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni.
Serikali ya mjini Kinshasa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda walisaini mjini Doha mwezi Julai makubaliano yanayolenga kuleta amani ya kudumu Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.