SiasaBurundi
Serikali mpya ya Burundi yaapishwa mjini Bujumbura
6 Agosti 2025Matangazo
Mawaziri 10 kati ya 13 ni wapya na wote ni kutoka chama tawala CNDD-FDD. Miongoni mwa walioteuliwa ni jenerali wa zamani wa polisi Leonidas Ndaruzaniye ambaye sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, huku Waziri wa zamani wa biashara, Marie Chantal Nijimbere, akiwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Burundi kuwa Waziri wa Ulinzi.
Mwezi Juni, Burundi ilifanya uchaguzi wa wabunge ambapo chama tawala CNDD-FDD, kilichopo madarakani kwa miaka 20, kilishinda kwa asilimia 96 na kuchukua viti vyote katika Bunge la Kitaifa. Upinzani, mashirika ya kutetea haki za binadamu na Kanisa Katoliki walikosoa na kusema uchaguzi huo uligubikwa na dosari kubwa.