Serikali kuu ya Ujerumani kuamua kutumwa wanajeshi mashariki ya kati
13 Septemba 2006Matangazo
Baraza la mawaziri la serikali kuu ya Ujerumani linatazamiwa kuamua hii leo juu ya kujumuishwa wanajeshi wa Ujerumani katika juhudi za kusimamia utaratibu wa amani kati ya Israel na Libnan.Ujerumani imependekeza kuongoza manuari za kimataifa zitakazopiga doria kulinda fukwe za Libnan.
Uamuzi wa bunge la shirikisho katika suala hilo,hautarajiwi kabla ya wiki ijayo.Katika wakati ambapo waliberali wa FDP wanapinga kutumwa wanajeshi wa Ujerumani mashariki ya kati,walinzi wa mazingira wanasema wataunga mkono pendekezo la serikali kuu ya Ujerumani la kutuma wanajeshi 2400 katika eneo hilo..