Scholz: Ushuru wa Trump ni makosa makubwa
3 Aprili 2025Matangazo
Kansela anayeondoka wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kimsingi ushuru mkubwa aliouweka Rais Trump kwa mataifa duniani ni makosa huku Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Bayrou akidai kwamba ushuru huo ni janga kwa dunia.
Naye Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema ushuru huo ni pigo kubwa kwa uchumi wa dunia.
Trump amesema ushuru huo kwa bidhaa zinazoingia Marekani ambao ni kati ya asilimia 10 hadi 49, utazifanyia washirika wa kibiashhara wa Marekani kile ambacho wamekuwa wakiifanyia Marekani kwa muda mrefu.