Scholz: Navalny alikufa kwa kupigania demokrasia ya Urusi
16 Februari 2025Katika mtandao wake wa X Scholz alisema Rais wa Urusi Vladimir Putin anapambana kubana uhuru na wale wanaoutetea, akisema kazi ya Navalny ilikuwa ya kijasiri zaidi.
Alexei Navalny mpinzani mkubwa wa rais Putin aliyefanya kampeni kubwa ya kuangazia ufisadi uliokuwa unafanyika nchini humo, alikufa mwaka mmoja uliopita akiwa gerezani alikokuwa anashikiliwa. Tangu wakati huo Urusi haijawahi kuzungumzia kwa uwazi kifo hicho.
Mwili wa Alexei Navalny wazikwa Moscow
Wafuasi wake wamepamga kumkumbuka Navalny kwa kutembelea kaburi lake mjini Moscow. Hata hivyo baadhi ya vituo vya telegram vinavyoiunga mkono Urusi vimewaonya wafuasi hao dhidi ya kuzuru kaburi la Navalny.
Matukio mengine ya kumkumbuka kiongozi huyo wa upinzani yatafanyika mjini Berlin anakoishi uhamishoni mkewe Yulia Navalnaya pamoja na wapinzani wengine wa serikali ya Urusi.