Scholz aonya ushirika wa CDU/CSU na AfD muswada wa uhamiaji
29 Januari 2025Matangazo
"Na ninasema kwa uwazi kabisa: ni lazima tuuzuie wingi wa wahafidhina wa CDU/CSU na wale wa AfD wa mrengo wa kulia, kuliunda bunge la Ujerumani, vinginevyo kutakuwa na serikali katika nchi hii, ambayo hakuna mtu atakayekuwa anaitaka." amesema Kansela Scholz.
Amesema kumekuwepo na makubaliano ya wazi miongoni mwa vyama vya kidemokrasia ndani ya bunge kwamba sera zao hazitangamani na vyama vya mrengo mkali wa kulia, tangu ilipoanzishwa Jamhuri ya Muungano wa Ujerumani zaidi ya miaka 75 iliyopita.Bunge la ujerumani lajadili sera kali za uhamiaji
Kiongozi wa upinzani Friedrich Merz kwa upande wake amesema demokrasia ya Ujerumani iko hatarini kufuatia mkwamo katika sera ya uhamiaji na usalama.