Scholz aonya kuhusu mustakabali wa Ulaya
28 Juni 2025Katika hotuba yake Scholz alijikosoa kwa uwazi lakini pia alitetea sera za serikali yake, akisisitiza kuwa hatua zilizochukuliwa zilikuwa sahihi kwa wakati wake. Aidha kansela huyo wa zamani alionya dhidi ya matumaini yasiyo halisi kuhusu Rais wa Urusi, Vladimir Putin, akisema kuwa kiongozi huyo anataka kuendeleza uvamizi wake nchini Ukraine na hata kutanua udhibiti zaidi.
Katika wito wa mshikamano wa kitaifa, Scholz amewataka matajiri kuchangia zaidi katika kugharamia ulinzi wa taifa, akishangazwa na mijadala ya kupunguza kodi kwao.
Wakati huohuo, Kamishna Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi, alieleza masikitiko yake kuhusu uamuzi wa Ujerumani kujiondoa kwa muda katika mpango wa kimataifa wa kuwahamisha wakimbizi. Akionya dhidi ya kuwarudisha kwa nguvu wakimbizi wa Syria, kwasababu serikali mpya ya Syria haina uzoefu wa kuwashughulikia na hali bado ni tete.