MigogoroSyria
Ripoti:Watoto 400,000 Syria hatarini kukabiliwa na utapiamlo
18 Aprili 2025Matangazo
Hali hiyo ni baada ya hatua ya Marekani kusitisha msaada, na kulilazimisha shirika hilo kupunguza operesheni zake katika nchi hiyo.
Bujar Hoxha, mkurugenzi wa Shirika hilo nchini Syria ameitolea wito jumuiya ya kimataifa kujaza haraka pengo la ufadhili lililoachwa na Marekani, akitahadharisha kwamba mahitaji ni "ya juu zaidi kuliko hapo awali" hasa baada ya miaka ya vita na kuporomoka kwa uchumi.
Mzozo uliodumu kwa zaidi ya miaka 13 nchini Syria uliiharibu vibaya nchi hiyo, huku mfumo wa afya ukivurugika na miundombinu kuharibika.
Mapema mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP lilikadiria kuwa Wasyria tisa kati ya 10 sasa wanaishi katika umaskini na wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.