Saudi Arabia yazindua mradi wa ujenzi mpya wa Damascus
7 Septemba 2025Saudi Arabia imekuwa mfadhili mkuu wa serikali mpya ya Syria, iliyochukua madaraka baada ya kuondolewa madarakani, mtawala wa muda mrefu Bashar al-Assad mwezi Desemba uliopita.
Katika hafla iliyofanyika leo mjini Damascus, Kituo cha Msaada wa Kibinadamu na Msaada cha Mfalme Salman (KSrelief) kilichopo chini ya serikali ya Saudi Arabia kilitangaza mpango wa msaada unaojumuisha mradi wa kuondoa zaidi ya mita za ujazo 75,000 za vifusi kutoka mji mkuu na vitongoji vyake.
Rais wa shirika hilo Abdullah Al Rabeeah na waziri wa usimamizi wa dharura na majanga wa Syria, Raed al-Saleh, walitia saini makubaliano ya mpango huo, unaojumuisha pia mipango ya kuchakata upya angalau mita za ujazo 30,000 za vifusi kutoka nyumba na majengo yaliyoharibiwa.
Saleh alisema vifusi hivyo vinazuia juhudi za kibinadamu na ujenzi upya, na akaonya kuwa mabaki ya silaha ambazo hazijalipuka bado ni tishio kwa maisha ya raia.