Saudi Arabia yataka Israel ishinikizwe iruhusu misaada Gaza
11 Aprili 2025Matangazo
Saudi Arabia imetaka shinikizo zaidi kuhakikisha uepelekaji wa misaada unaendelea bila kutatizwa katika Ukanda wa Gaza kufuatia hatua ya Israel ya kuzuia uingizaji wa mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Hayo yamesemwa leo na waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan baada ya mkutano wa kikanda wa washirika uliofanyika kusini mwa Uturuki.
Kauli yake inakuja baada ya shambulizi la alfajiri la kutokea angani lililofanywa na jeshi la Israel kuwaua watu kumi wa familia moja, wakiwemo watoto saba, katika mji wa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Gaza.