Sane kuihama Bayern mkataba wake utakapokwisha
11 Juni 2025Sane alisafiri na Bayern Munich kuelekea Marekani kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia la Vilabu, linaloanza siku ya Jumamosi, ingawa kandarasi yake inafikia mwisho Juni 30 - wiki chache kabla fainali ya mashindano hayo mnamo Julai 13.
Kulingana na shirika la habari la Sky, Bayern ilimpendekezea Sane kandarasi mpya yenye mshahara mkubwa zaidi ila akaikataa. Amehusishwa sasa na kuhamia Galatasaray na Fenerbahce. Arsenal pia wanaripotiwa kumtaka Sane.
Lakini ripoti nyengine zinaarifu kwamba Galatasaray ndio walio katika nafasi nzuri ya kuipata saini ya winga huyo raia wa Ujerumani.
Sane alijiunga na Bayern kutoka Manchester City mwaka 2020 kwa dau la dola milioni 57.1 na ni mmoja wa wachezaji wa Bayern wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi na baada ya mazungumzo magumu, anadaiwa kukataa kuupunguza mshahara wake pakubwa.