Sane andoka Bayern na kujiunga na Galatasaray
30 Juni 2025Winga huyo wa Kijerumani sasa ni mchezaji wa Galatasaray ya Uturukikuanzia Jumanne huku Bayern ikiendelea kucheza Kombe la Dunia la Vilabu nchini Marekani.
Sane alishindwa kufunga bao alipobaki yeye na kipa wa Agustin Rossi katika dakika za mwisho za ushindi wa Bayern wa 4 – 2 wa mechi ya hatua ya 16 za mwisho dhidi ya Flamengo mjini Miami.
Mwanachama wa bodi anayehusika na michezo Max Erbel alitangaza hafla ya kumuaga Sane Jumatatu katika kambi ya mazoezi ya timu hiyo jimboni Florida, akisema: "Ilikuwa muhimu kwamba alikuwepo. Tunashukuru kwamba alihudhuria."
Sane, mwenye umri wa miaka 29, alisaini mkataba na Galatasaray hadi 2028 kabla ya kuanza kwa mashindano ya FIFA. Alichaguliwa na kocha Vincent Kompany katika kikosi cha kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu hata ingawa ilikuwa wazi kuwa hatokuwa nao hadi hatua za mwisho mwisho.
"Ni jambo la kipekee kwenye mashindano kwamba hauwezi kucheza hadi mwisho," alisema Sane baada ya dakika zake za mwisho katika uzi wa Bayern.
Lakini aliongeze: "Nimefurahi sana wiki hizi mbili nilizokuwa hapa kwa sababu ni kikosi cha kipekee chenye umoja. Nilikuwa na furaha kuwa uwanjani na wenzangu.
dpa