Sane ajiunga na Galatasaray kwa mkataba wa miaka 3
12 Juni 2025Matangazo
Galatasaray ambao ndio mabingwa wa Uturuki walithibitisha katika mtandao wa kijamii kwamba Sane amewasili Istanbul kwa mazungumzo ya kujiunga nao.
Sane sasa ameihama Bayern kabla kukamilika kwa kandarasi yake mwishoni mwa mwezi huu baada ya mazungumzo kuhusu mkataba mpya kuchukua muda mrefu na mwafaka kutofikiwa.
Bayern katika kipindi hicho chote lakini walikubaliana na Jamal Musiala na Joshua Kimmich kuhusiana na kuwaongezea mkataba.
Huo ndio mwisho wa Sane hapo Bayern baada ya kujiunga nao kutoka Manchester City mwaka 2020.