Sanchez na Sissi wapinga mpango wa kuwahamisha wapalestina
19 Februari 2025Wamesema mpango huo ni sawa na kuwahamishaji kwa lazima watu hao na pia ni kinyume cha maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Wakiwa pamoja katika ukumbi wa Palacio de la Moncloa, Sánchez alisema haungi mkono pendekezo la kuwahamisha wapalestina kutoka Gaza.
"Nataka kusisitiza, kama nilivyosema faraghani na pia kwa ujumbe wa mawaziri wa Misri, kukataa vikali kwa Uhispania na serikali yake juu ya pendekezo la kuwahamisha Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza," Sanchez aliyasema hayo baada ya mkutano waliofanya wakati wa ziara rasmi ya Al Sisi nchini Uhispania.
Mataifa yaomba mkutano wa dharura kuangazia hali katika Ukanda wa Gaza
Kwa upande wake, Al Sisi ambaye yuko katika ziara yake ya pili rasmi nchini Uhispania, alimshukuru Sánchez kwa msimamo huo wa Uhispania wa kutambua haki za Wapalestina na pia kwa kuanzishwa kwa taifa la Palestina.