SANAA.Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen atarajiwa kunyakuwa ushindi mkubwa
22 Septemba 2006Matangazo
Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh anatarajiwa kuwa mshindi baada ya kunyakuwa kiwango kikubwa cha kura katika uchaguzi uliofanyika nchini humo siku ya jumatano.
Msemaji wa tume ya uchaguzi ya Yemen ameeleza kuwa rais Ali Abdullah Saleh amepata asilimia 80 ya kura zilizohesabiwa dhidi ya mpinzani wake aliyekuwa waziri wa mafuta Faisal Bin Shamlah aliyepata asilimia 20 pekee.
Ali Abdallah Saleh ameiongoza Yemen kwa kipindi cha miaka 28 iliyopita.
Wasimamizi wa kigeni wameutaja uchaguzi wa nchi hiyo kuwa ulikuwa wa mafanikio makubwa licha ya kuwepo matatizo machache.
Watu watano waliuwawa siku ya kupiga kura baada wafuasi wa rais Saleh kukabiliana na upande wa upinzani.