SANAA. Wayemeni 7 kuachiliwa kutoka jela ya Guantamobay
1 Agosti 2005Matangazo
Marekani imekubali kuwaachilia huru wafungwa 7 raia wa Yemen kutoka jela ya Guantanamobay.
Waziri wa mambo ya nje wa Yemen Abubakar al Qirbi amesema utawala wa Yemen umepokea mawasiliano kutoka Washington lakini tarehe maalum ya kuachiliwa wafungwa hao bado haijatangazwa.
Bwana Qirbi amesema kuwa Washington imeifahamisha Yemen kuwa kuna wafungwa wengine 107 raia wa Yemen kati ya wafungwa 510 waliozuiliwa katika jela ya Guantanamobay.
Taarifa kutoka makao makuu ya jeshi la Marekani Pentagon zime eleza kuachiliwa wafungwa wengine 7 wa kutoka Saudi Arabia, Afghanistan na Sudan mapema mwezi huu.
Yemen imejiunga katika harakati za kupambana na ugadi tangu shambulizi la Marekani la septemba 11 mwaka 2001.