SANAA. Ubalozi wa Marekani kufunguliwa leo nchini Yemen.
11 Aprili 2005Matangazo
Ubalozi wa Marekani nchini Yemen unatarajiwa kufunguliwa tena hii leo baada ya hatua za dharura za kukabiliana na mashambulio ya kigaidi kuchukuliwa. Ubalozi wa Uingereza nchini humo ulifunguliwa tena hapo jana baada ya kufungwa kwa siku moja kufuatia hofu ya mashambulio ya wanamgambo katika taifa hilo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la nchi hiyo, waasi waislamu wa madhehebu ya Shia wasiopungua 40 wameuwawa katika mapigano kazkazini mashariki mwa nchi hiyo tangu Ijumaa iliyopita. Mapigano ya hivi punde yamesababisha idadi ya vifo kupindukia 270 katika majuma mawili yaliyopita. Wanajeshi wa serikali wanajaribu kuwasaka wafuasi wa mhubiri aliyeuwawa Sheikh Hussein Badr Eddin al-Huthi.