SANAA : 39 wauwawa katika maandamano ya kupinga kupanda bei ya mafuta
22 Julai 2005Takriban watu 39 wameuwawa katika siku mbili za ghasia nchini Yemen ambapo watu walikuwa wakiandamana kupinga kupanda kwa bei za mafuta.
Miongoni mwa watu waliopoteza maisha yao ni askari wa usalama.
Waandamanaji 50 wamejeruhiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa na katika miji mengine sita kusini na kaskazini ya nchi hiyo huko wanajeshi wakisaidiwa na vifaru na magari ya deraya wakiwa wamewekwa kwenya barabara kuu.
Vifaru vya kijeshi vilivyowekwa kuwasaidia polisi vimeonekana karibu na majengo ya serikali wakati hatua kali za usalama zimechukuliwa katika maeneo wanakoishi maafisa waandamizi wa serikali.
Bei za mafuta nchini humo ziliongezeka karibu maradufu hapo Jumanne wakati serikali ilipoondowa ruzuku zake kwa bidhaa za mafuta.