Salvini: Ninatumai kuiona Urusi michezo ya Olimpiki 2026
25 Machi 2025Matangazo
Salvini amesema kwa kuzingatia kwamba mazungumzo ya amani kuhusu vita vya Ukraine yanaendelea kwa sasa, na kwamba lengo la michezo hiyo ya Olimpiki linapaswa kuwa kile kinacholeta watu na wanariadha pamoja, anatumaini kwamba mashindano hayo ya Milan-Cortina 2026 yatakuwa Olimpiki ya kwanza kuwaona wanariadha wa Ukraine na Urusi wakishiriki.
Urusi na mshirika wake Belarus wamepigwa marufuku kuandaaa mashindano ya michezo ya kimataifa tangu uvamizi wa Urusi wa Februari 2022 nchini Ukraine, huku bendera, nyimbo zao za taifa pamoja na maafisa wao wakipigwa marufuku kushiriki mashindano mengi ulimwenguni.