SAFARI ZA NDEGE ZA KIRAIA ZASITISHWA IRAQ:
24 Novemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Muungano unaoongozwa na Marekani nchini Iraq umeamaua kusitisha misafara yote ya ndege za kiraia mjini Baghdad.Uamuzi huo umepitishwa siku moja baada ya ndege ya kubebea mizigo ya Kijerumani ya shirika la DHL kupigwa na kombora lililorushwa kutoka nchi kavu muda mfupi tu baada ya kuondoka uwanjani.Ingawa bawa la ndege hiyo lilishika moto,ndege ilifanikiwa kutuwa kwa dharura bila ya mtu ye yote yule kujeruhiwa.Shirika la DHL husafirisha barua kwa wanajeshi wa Kimarekani walio nchini Iraq.Kwa mujibu wa msemaji wa Kimarekani,jeshi linafanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo.