Safari ya Uganda kujitosa katika biashara ya mafuta
8 Aprili 2025Kundi la vijana wanaoandamana mara kwa mara kwenye barabara za mji wa Kampala wanapinga shughuli za ujenzi wa bomba la mafuta la EACOP pamoja na miradi husika likielezea kuwa itaathiri mazingira. Lakini serikali ya Uganda imeazimia kuendelea na mpango huo ambao ni moja ya mikakati iliyoanza kuzingatiwa wakati mafuta yalipoguduliwa mwaka 2006.
Uchimbaji mafuta ni kazi ambayo inaweza kufanywa hata na wanawake na ikiwa utaisomea, basi anaweza kufanya kila jambo. Linnet Nayiga ni miongoni mwa vijana wa kike ambao baada ya kupata mafunzo sasa wanasimamia shughuli za uchimbaji mafuta katika visima vya Tilenga katika mbuga za Wanyama za Murchison.
Uganda kuzindua awamu ya tatu ya utoaji leseni ya utafiti wa mafuta
"Uchimbaji mafuta ni kazi ambayo inaweza kufanywa hata na wanawake na wakati ukiamua kuisomea basi unatarajia kufanya kila jambo," alisema Tilenga.
Hata hivyo, kizingiti kikubwa kinachofanya ndoto ya Uganda kutotimia ni kupata wawekezaji walio na mtaji ili kufanikisha ujenzi wa miundombinu ya kuchimba na kusafisha mafuta. Hii ni kutokana na wanaharakati wa mazingira na haki za binaadamu kuanza kuupinga mradi huo, jambo lililopelekea benki na mashirika mengi kusita kuufadhili kwa njia ya mkopo.
Yapi manufaa ya uganda kuwa na mtambo wa kusafisha mafuta?
Makampuni ya Total Energies ya Ufaransa na CNOOC ya China yaliendelea kuwa na imani kwamba mradi huo ungefanikiwa na yakaendelea kuwekeza katika miundombinu muhimu na kubaini visima vya mafuta na kujenga mabomba ya kutoa mafuta ghafi kutoka ardhini. Mhandisi Mike Mugerwa ambaye ni meneja mkuu wa shirika la kitaifa la kuchakata mafuta la Uganda amelezea manufaa ya Uganda kuwa na mtambo huo
"Mtambo wa kusafisha mafuta pekee utailetea Uganda dola bilioni 3.4 kila mwaka ambao utachangia angalau asilimia 10 kwa pato la taifa na bidhaa zitakazotokana na shughuli hii, zitasaidia kuzalisha mbolea kwa ajili ya kilimo na kwa hiyo kuzidisha kiwango cha uzalishaji chakula," alisema bwana Mugerwa.
Mashirika yaushutumu mradi wa mafuta wa Uganda
Kulingana na kiwango cha mafuta kinachokisiwa kuwa mapipa bilioni 6.5 Magharibi mwa Uganda, ilitabiriwa kuwa mafuta hayo yangeleta faida kubwa ikiwa yangeuzwa kwenye soko la kimataifa. Hapo ndipo Uganda ilijadili na Tanzania kuhusu ujenzi wa bomba la umbali wa kilomita 1,440 chini ya mradi ujulikanao kama EACOP kati ya pwani ya Tanga na eneo la Bunyoro ambapo mafuta hayo yatachimbwa.
Je mradi huo unaweza kuharibu mazingira?
Na ndipo mradi huo unaotarajiwa kugharimu takriban dola bilioni 5 ulipoanza kupingwa na makundi ya wanaharakati ndani na nje ya nchi kwa madai kuwa bomba hilo litapita katika manaeno ya mbuga za wanyama na makaazi ya watu na hivyo kusababisha uharibifu wa uoto wa asili na pia kukiuka haki za binadaamu. Samuel Wanda ni mmoja wa wanaharakati wa kulinda mazingira.
"Ujenzi wa bomba unaoendelea na pia huo mtambo wa mafuta vinaathiri mazingira na ndiyo maana tunavipinga," alisema Samuel Wanda.
Wanaharakati wanaopinga mradi wa mafuta Uganda wakamatwa
Lakini Gloria Sebikari msemaji wa Mamlaka ya mafuta ya Uganda PAU anafafanua kuwa miradi hiyo miwili imelengwa kuwezesha biashara ya mafuta kunufaisha Uganda kwa kutosheleza mahitaji na nchi na pia mauzo kimataifa
"EACOP na mtambo wa kusindika mafuta ni muhimu katika kuendesha biashara ya mafuta ili Uganda ipate dola bilioni 2 kila mwaka kutokana na uzalishaji ," alisema Sebikari.
Hivi majuzi, kampuni kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ilisaini mkataba wa kuwekeza katika mtambo huo wa kuzalisha mapipa 60,000 ya mafuta kila siku na sasa kuna matarajio kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja, biashara ya mafuta itaanza. Kwa sasa zaidi ya visima 100 vya mafuta vimechimbwa eneo la Hoima na Buliisa.